Nicolas Maduro amelaani vikali mauaji yanayotekelzwa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kuyafananisha na jinai za kutisha zaidi katika historia.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Maduro alielezea hatua ya jeshi la Israel kulenga kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza mauaji ya umati na kuongeza kuwa hivi sasa katika eneo zima la Ukanda wa Gaza Israel inatekeleza mauaji ya kimbari ya kutisha zaidi ambayo ubinadamu umeshuhudia tangu wakati wa Hitler."
"Amebainisha masikitiko yake kuwa Israel inaendeleza mauaji ya kimbari tika Ukanda wa Gaza mbele ya macho ya ulimwengu bila mtu yeyote kuizuia."
Aliikosoa Marekani na Umoja wa Ulaya na kusema pamoja na kuwa pande zote mbili zina uwezo lakini "hazifanyi lolote kukomesha mauaji haya". Maduro ameendelea kusema kuwa: "Kwa maoni yangu, wao ni washirika katika mauaji haya."
Pia alimshutumu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kupuuza sheria za kimataifa na kufanya ukatili dhidi ya watoto Waislamu na Wakristo huko Palestina.Mashambulizi ya anga ya Israel, Jumapili jioni, yalisababisha vifo vya Wapalestina 45 waliokimbia makazi yao, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Israel inaendelea na mashambulizi yake ya kikatili huko Gaza licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki wiki iliyopita kuiamuru "kusitisha mara moja" mashambulizi yake huko Rafah.
Takriban Wapalestina 36,100 wameuawa huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine zaidi ya 81,000 wamejeruhiwa tangu Oktoba.
342/